Wizara ya afya imetoa kondomu 3,000 kwa waathiriwa wa mafuriko zaidi ya 6,000 walioko katika kambi katika Shule ya Garashi, kaunti ya Kilifi.
Kwenye taarifa ya vyombo vya habari ,Waziri wa Afya Dkt Anisa Omari amesema mbali na kondomu hizo wamezidisha huduma za afya kwa waathiriwa wote walioko kambi ya Garashi.
‘’Tumepeleka kondomu 3,000 kwa waathiriwa hao walioomba wapewe.mbali na mipira hiyo tumeweka kliniki katika mojawapo ya madara katika shule hiyo’’amesema Dkt Omari na kuongeza kwamba
“Vilevile tumempeleka wafanyakazi wanaotoa huduma za afya mchana na usiku, na tutaendelea kuwahudumia wakazi hao mpaka hali itakapoimarika na warudi makwao, ’’amesema Dkt Omari.
Wananchi hao zaidi ya 6,000 walioathiriwa na mafuriko katika eneo la Malindi waliomba kusambaziwa mipira hiyo ili kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwamo ukimwi.
Wakizungumza na waandishi wa habari wamesema kwamba kwa sababu wako wengi kuna vijana ambao bado damu zinachemka,kuna hatari miongoni mwao kuanza kufanya mapenzi na hivyo basi kuzua hofu ya kupata magonjwa.
“’Tunahitaji kuletewa mipira ya kondomu kwa sababu tumekuwa wengi hapa na hatujui wengine wako na hali gani.Pengine umekutana na mtu wako ambaye mlikuwa mkiendelea naye huko nje. Sasa ni balaa.Ni afadhali ziletwe kwa wingi ziweze kusaidia.Yote ni mambo na afya tu,’’amesema mwanamke mmoja ndani ya kambi hiyo
Ofisa Mkuu wa Afya katika kaunti ya Kilifi Kenneth Kazungu amesema kuwa Serikali inapanga kuwapelekea kondomu nyingi zaidi.
“Ni kweli watu wanapokuwa pamoja na katika mazingira hayo huwa kuna hofu ya kiafya na sisi kama Serikali tunawapelekea kama wanavyotaka.Tuna kondomu za kutosha katika bohari yetu na hiyo ni mojawapo ya mikakati ya kuhakikisha afya bora kwa kila mwananchi,’’amesema Mwanamke huyo.

No comments:
Post a Comment