Kikwete atoa sababu za kutohudhuria katika sherehe za kuapishwa kwa Kenyatta. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 28 November 2017

Kikwete atoa sababu za kutohudhuria katika sherehe za kuapishwa kwa Kenyatta.

 
 Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushindwa kuudhuria sherehe hizo.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter Mhe. Kikwete amempongeza Rais Kenyatta kwa ushindi alioupata na kumshukuru kwa kumualika katika sherehe hizo ila ameshindwa kuhudhuria kutokana majukumu alionayo kwa sasa.

Nakupongeza Rais @UKenyatta kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi rafiki ya Kenya. Nakushukuru kwa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwako. Nasikitika sitaweza kuhudhuria kutokana na kuingiliana kwa majukumu. Nakutakia kila la kheri katika awamu yako ijayo.

Katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Kenyatta Tanzania inawakilishwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Popular