Mchungaji Msigwa afunguka mengi kuhusu Rais Magufuli. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 3 May 2018

Mchungaji Msigwa afunguka mengi kuhusu Rais Magufuli.

 
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amefagilia utendaji kazi wa Rais John Magufuli kwamba amekuwa akitekeleza majukumu yake bila kubagua vyama vya siasa, huku akitolea mfano jinsi fedha za miradi mbalimbali zinavyomiminika jimboni kwake.

Mchungaji Msigwa ametoa kauli hiyo Jana Mei 2, 2018 katika Ikulu ndogo ya Iringa kwenye hafla fupi ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Rais Magufuli.

Hata hivyo, Mchungaji Msigwa alipozungumza na kulunzifikra blog  leo Mei 3, 2018  kuulizwa kuhusu video inayosambaa ikionyesha akimwagia sifa kiongozi mkuu huyo wa nchi, amesema ni kweli ila video hiyo imekatwa na kuna mambo aliyoyazungumza, ikiwamo wanachama mbalimbali wanaohamia CCM.

Wakati akizungumza katika hafla hiyo Mchungaji Msigwa amesema, “Mhe Rais Magufuli  umekuwa ukisisitiza katika hotuba zako kuwa hujali vyama na hilo limekuwa likidhihirika hujali vyama. Umesaidia sana bahati mbaya hawakukupangia ratiba ya kufungua miradi, hela za kutoka kwako zimekuja nyingi.”

“Amezungumza Mahiga (Balozi Augustine-Waziri wa Mambo ya Nje) tuna barabara nzuri katika kipindi chako ambacho umekuwa rais. Tumejenga barabara ya lami mradi wa Benki ya Dunia kutoka Mlandege mpaka kwa mkuu wa wilaya karibu Sh3.5bilioni.”

Katika maelezo yake ya leo kuhusu kauli yake hiyo,  Mchungaji Msigwa amesema katika video hiyo, hakuna kipande ambacho aliwazungumzia watu wanaohama vyama, kubainisha kuwa wanaotoka upinzani kwenda CCM hawana sababu ya kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment

Popular