Ule mjadala wa hali ya afya ya akili ya Rais Donald Trump, unaweza kuibuka tena baada ya daktari wake binafsi kusema hakuandika barua iliyoeleza kuwa kiongozi huyo hana matatizo ya akili.
Mjadala kwamba Trump anaugua ugonjwa wa akili ulizimwa baada ya barua hiyo kutoka ikiwa imesainiwa na daktari wake binafsi, Dkt Harold Bornstein.
Jana (Jumanne Mei mosi), Dkt Bornstein aliiambia CNN kuwa hakuandika barua hiyo ambayo timu yake ya kampeni iliitumia kujenga hoja kuwa iwapo angechaguliwa, Trump angekuwa "rais mwenye afya bora kuwahi kuchaguliwa".
“Alilazimisha barua kuandikwa. Sikuandika ile barua," alisema Dkt Bornstein.
Barua hiyo yenye aya nne ilisema “afya yake (Trump) ni nzuri sana, hasa akili yake".
“Kama akichaguliwa, Trump, naweza kueleza kwa kauli thabiti, atakuwa mtu mwenye afya nzuri sana kuwahi kuchaguliwa kuwa rais," inasema barua hiyo.
Siku kadhaa kabla ya barua hiyo kutoka, Trump mwenyewe alisema mapema kile ambacho Dkt Bornstein angekisema.
Kauli ya Dkt Bornstein kuwa Trump, ambaye wakatyi huo alikuwa mgombea, alimuagiza kitu cha kuwaambia waandishi wa habari kuhusu afya yake, imekuja siku moja pamoja na habari nyingine inayomuhusisha daktari hiyo na kupewa umuhimu mkubwa na vyombo vya habari.
Katika mahojiano na NBC, Dkt Bornstein alisema asubuhi ya Feb 3, 2017, mlinzi wa muda mrefu wa Trump, mwanasheria mmoja wa kampuni ya Trump na mtu mwingine walivamia ofisi yake iliyoko Manhattan, wakaondoa taarifa zote za afya ya rais huyo, kitu ambacho daktari huyo amesema kilimfanya ajione amebakwa, mwenye hofu na fedheha.”
Kwenye mkutano na waandishi jana asubuhi, katibu wa Ikulu, Sarah Sanders alipuuza madai kuwa ofisi ya daktari huyo ilivamiwa, akisema “taarifa zilikuwa zikihamishiwa kwenye Kitengo cha Afya cha Ikulu, kama ilivyoombwa.”

No comments:
Post a Comment