Pluijm afunguka mengi juu ya mechi yake dhidi ya Yanga. - KULUNZI FIKRA

Saturday 3 March 2018

Pluijm afunguka mengi juu ya mechi yake dhidi ya Yanga.

 
KOCHA wa Singida United, Hans van Der Pluijm amesema hana wasiwasi kupangwa na Yanga katika robo fainali ya Kombe la FA lakini anataka kuifunga Azam FC kwanza katika Ligi Kuu Bara.

Leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, Azam itakuwa mwenyeji wa Singida United katika mechi ya ligi kuu inayotarajiwa kuwa ngumu.

Azam ipo nafasi ya tatu katika ligi ikiwa na pointi 35 huku Singida United ikiwa nafasi ya nne na pointi 34, hivyo mshindi anaweza kujiimarisha zaidi katika msimamo.

Kocha Pluijm ameiambia kulunzifikra blog kuwa: “Tunafahamu ubora wa Azam, tutatilia mkazo zaidi katika mechi hiyo na tunaamini tutatengeneza nafasi zaidi za kujipatia ushindi.”

Akizungumzia ratiba ya mechi za robo fainali za Kombe la FA iliyopangwa jana ambapo watacheza na Yanga ambayo amewahi kuifundisha, kocha Pluijm alisema, hawana wasiwasi kwani anaijua timu hiyo vizuri.

“Sina wasiwasi na ratiba kwani Yanga naijua, tunajitengenezea mazingira ya ushindi ili tujiweke katika nafasi ya kupata tiketi ya mechi za kimataifa msimu ujao,” alisema kocha  Pluijm raia wa Uholanzi.

Bingwa wa Kombe la FA anapata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika huku bingwa wa ligi kuu akishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika

No comments:

Post a Comment

Popular