Tundu Lissu afunguka mengi. - KULUNZI FIKRA

Wednesday 21 February 2018

Tundu Lissu afunguka mengi.

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya (Chadema) Mhe Tundu Antiphas Lissu amefunguka na kusema amefarijika sana kutembelewa na Mbunge wa Tandahimba (Cuf) Katani Ahmad Katani na kudai mbunge huyo alikuwa miongoni mwa watu waliompeleka Nairobi.

Mhe Tundu Lissu ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii na kusema mbali na kumlijuana hali lakini waliweza kujadiliana kuhusu mwenendo wa siasa zinazoendelea nchi Tanzania.

"Mhe Katani amekuja Ubelgiji kunijulia hali pamoja na kuja kujadiliana nami masuala mbali mbali yanayohusu siasa za nchi yetu na mustakbali wa Taifa letu. Katani alikuwa kwenye msafara wa Wabunge walionipeleka Nairobi, Kenya, mara baada ya jaribio la mauaji la September 7, na alikaa Nairobi kwa siku nne. Nimefarijika sana na ugeni huu wa ndugu yangu na kaka yangu Katani", amesema Mhe Tundu Lissu.

Mhe Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana tangu Septemba 7,2017 akiwa mkoani Dodoma, na kisha kupelekwa nchini Nairobi kwa matibabu na baada ya miezi 3 alipelekwa nchini Ubelgiji kwa hatua nyingine ya matibabu.

No comments:

Post a Comment

Popular