Askofu KKKT: Viongozi wa dini wanaongea siasa 2000 sasa , Haiwezekani kutenganisha siasa na dini - KULUNZI FIKRA

Thursday 22 February 2018

Askofu KKKT: Viongozi wa dini wanaongea siasa 2000 sasa , Haiwezekani kutenganisha siasa na dini

Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe, Askofu Benson Bagonza, amesema amani ni jambo linalopaswa kuhubiriwa na vyama vya siasa na taasisi za dini.

Amesema kwamba hawezi kusema viongozi wa dini wasishiriki katika siasa wakati kila kitu wanachofanya kinatokana na siasa.

Askofu  Benson Bagonza alisema hayo Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania TCD, ambao ulihuisha pia viongozi wa dini.

Alisema viongozi wa dini wana wajibu wa kushauri na kuonya pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani, hivyo kujitenganisha na siasa haitawezekana.

"Hatuwezi kukaa katika nchi kama tupo peponi, yapo matukio ya uvunjifu wa amani ambayo yanatokea yanayohusu uvunjifu wa amani nchini lazima tukemee" alisema Askofu Benson.  Boganza.

"Kauli hii ni ibada ya sanamu, hili shati nililovaa bei imepangwa na wanasiasa, kukubali kununua nimeshashiriki siasa, ni kitu kisichowezekana unakula, unalala, unaamka hii ni siasa, kwa hivyo tunaishi katika nchi ya siasa", alisema Askofu Benson Boganza.

"Kanisa lina nguvu karibu miaka 2000, hivi vyama hakuna kilichofikia hata miaka mia, maana hii habari ya viongozi wa dini kuongelea siasa imekuwepo kwa miaka 2000 sasa", alisema Askofu Benson Boganza.

No comments:

Post a Comment

Popular