Salum Mwalimu atoa malalamiko kwa Tume ya Uchaguzi. - KULUNZI FIKRA

Saturday 17 February 2018

Salum Mwalimu atoa malalamiko kwa Tume ya Uchaguzi.

Mgombea wa ubunge jimbo la Kinondoni kupitia Chadema, Salum Mwalimu amelalamikia uchaguzi huo kuwa mawakala wa chama hicho wamezuiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura kwa wakati.

Salum Mwalimu alitolea mfano Kata ya Hananasifu kuwa mawakala hao wameingia saa 2 asubuhi wakati vituo vyote 613 vya kupigia kura vimefunguliwa saa 1 asubuhi.

Salum Mwalimu ambaye alitembelea kituo cha Hananasifu B, amesema mawakala hawa wamezuiwa baada ya kuelezwa kwamba hawana fomu za halmashauri na wengine zile za kiapo

"Cha ajabu nimeingia kituo kimojawapo halafu wakala wa chama cha UMD anazo barua zote tangu saa 12 asubuhi wakati huohuo wakala wa Chadema hana barua na nilipohoji wananiambia mbona wakala wa CCM pia hana barua na hajaingia,” amesema Salum Mwalimu.

"Sasa mtu anapoanza kukuuliza mbona na wa CCM hana unaanza kujiuliza maswali mengi kwanini? Mle ndani walivyokaa wamejipanga kufanya wanachokifanya na wao wanajua wanafanya kazi kwa maelekezo ya nani.”amesema Salum Mwalimu.

No comments:

Post a Comment

Popular