Mambosasa atoa onyo Kali kwa chama cha Cuf. - KULUNZI FIKRA

Saturday 17 February 2018

Mambosasa atoa onyo Kali kwa chama cha Cuf.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa ametoa onyo kwa kikundi cha Wananchi(CUF) baada ya kudai kuwa wamepata taarifa kuwa kuna mtu ametuma kwenye mtandano kuwa vijana wa chama hicho wajikusanye kufanya fujo katika uchaguzi unaoendelea Kinondoni.

Kamanda Mambosasa ametoa onyo hilo leo katika uchaguzi mdogo unaoendelea Kinondoni na Siha amesema kuwa jeshi la polisi halitamvumilia yoyote atakayetaka kuvuruga uchaguzi huo.

“Kupitia kwenu naomba kutoa onyo kwamba tumepata taarifa kuwa kuna mtu amerusha kwenye mtandao kwamba vijana wa CUF wajikusanye waje kufanya fujo wakati wa kuhesabu na wakati wa kutangaza matokeo", amesema kamanda Mambosasa.

"Jeshi la polisi halitamvumilia yoyote atakayetaka kuvuruga uchaguzi huu ambao kimsingi tunakwenda kuumaliza salama ni kukosa ustaarabu na nikukosa utu na kutoitendea haki demokrasia inayompa uhuru Mtanzania yoyote kuchagua mtu anaempenda”, amesema Kamanda Mambosasa.

No comments:

Post a Comment

Popular