Chuo cha NIT chatoa udhibitisho kuhusu Mwanafunzi aliyepigwa risasi na polisi. - KULUNZI FIKRA

Saturday 17 February 2018

Chuo cha NIT chatoa udhibitisho kuhusu Mwanafunzi aliyepigwa risasi na polisi.

Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kimesema aliyepigwa risasi jana Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam na kufariki dunia ni mwanafunzi wa chuo hicho.

Chuo hicho kimemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Akwilina Akwiline aliyekuwa anasoma shahada ya kwanza ya ununuzi na ugavi.

Leo, Februari 17, 2018, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandamana jana.

Wafuasi hao wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mhe Freeman Mbowe waliandamana kuelelea ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.

Akizungumza na mwandishi wa kulunzifikra blog, Ofisa Uhusiano wa NIT, Ngasekela David amesema wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha wanafunzi huyo.

"Ni kweli alikuwa wanafunzi wetu na tumepokea kwa masikitiko taarifa hizi. Tunaendelea kufuatilia zaidi, "amesema David.

No comments:

Post a Comment

Popular