Jeshi la polisi lakana kumkamata Salum Mwalimu. - KULUNZI FIKRA

Saturday 17 February 2018

Jeshi la polisi lakana kumkamata Salum Mwalimu.

Kamanda wa Polisi wilaya ya Kinondoni, Jumanne Muliro amesema mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu hakukamatwa na Polisi, bali alijipeleka mwenyewe ili akamatwe wakati si mtuhumiwa.

Akizungumza na mwandishi wa kulunzifikra blog  leo Frebuari 17, 2018, Kamanda Muliro amesema mgombea huyo alijipeleka mwenyewe kwenye gari la Polisi wakati si mtuhumiwa, akiamini kuwa kitendo hicho kitawafanya waandishi wa habari kumpiga picha ili ionekane kuwa amekamatwa.

"Hizi ni hadithi za abunuwasi. Haya mambo ya kufikirika hayatakiwi kabisa. Yeye ameshapiga kura akae asubiri matokeo", amesema kamanda Muliro.

"Amelazimisha kuchukuliwa na kuingia kwenye gari wakati si mtuhumiwa".amesema kamanda Muliro.

Timu ya waandishi wa habari ilishuhudia leo saa 6 mchana, Salum Mwalimu akiondoka na Polisi katika Defender na kupelekwa katika kituo cha Magomeni ambapo alikaa kwa takribani robo saa na kuachiwa.

Salum Mwalimu alifika katika kituo hicho baada ya kusikia taarifa za baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakidai kuwa kuna mtu ameondoka na sanduku lenye kura, baadaye kukamatwa na Polisi akiwa na sanduku hilo.

No comments:

Post a Comment

Popular