Chadema yazungumzia kuhusu kujitoa uchaguzi wa Kinondoni. - KULUNZI FIKRA

Friday 16 February 2018

Chadema yazungumzia kuhusu kujitoa uchaguzi wa Kinondoni.

 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandaoni kuwa imejitoa katika uchaguzi mdogo wa marudio kwenye jimbo la Kinondoni, Siha na kata nane nchini na kuwataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo wazipatapo.

Akizungumza na mwandishi wa  kulunzifikra blog  Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- Chadema John Mrema amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kudai wanaofanya hivyo ni kundi cha watu wachache wenye lengo la kutaka kupotosha umma ili kesho wasiende kupigia kura.

"Taarifa hizo ni za uongo n zinasambazwa na watu ambao wameshashindwa naomba watu wazipuuze. Tunapozungumza sasa hivi Mwenyekiti wa chama Mhe Mbowe amehitimisha kampeni katika jimbo la Kinondoni na Mhe  Lowassa yeye amehitimisha  kampeni kule Jimboni Siha",amesema Mrema.

Pamoja na hayo, Mrema ameendelea kwa kusema "tunaomba kuwaambia wananchi na wanachama wa Chadema kuwa hiyo sio barua yetu na pia sio utaratibu kwa mujibu wa kanuni mwenyekiti wa chama kuandika barua ya kujitoa kama mtu mwenye haki ya kujitoa ni mgombea. Kwa hiyo hata hao watu walioandika hiyo barua hawajui sheria za uchaguzi zinasemaje".

Kwa upande mwingine, Mrema amezidi kuwasisitizia wananchi kuzipuuza taarifa zozote zinazotoka sasa kuhusu kutoshiriki uchaguzi huku akiwaomba wananchi katika Jimbo la Kinondoni na Siha kujitokeza kwa wingi kesho kushiriki kupiga kura kwa sababu ni haki yao ya msingi.

No comments:

Post a Comment

Popular