Padri amekamatwa kwa kujiusisha na mapenzi ya Jinsia moja. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 17 January 2018

Padri amekamatwa kwa kujiusisha na mapenzi ya Jinsia moja.

nchini Kenya imeripotiwa kumkamata Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Gonda, Kigumo anayeshutumiwa kufanya mapenzi na mwanamume mwenzake.

Polisi imesema jana kwamba wanakijiji wa Kaunti ya Murang'a katikati mwa Kenya wamekuwa wakimfuatilia Padri huyo ambaye wamekuwa wakimshuku kuwa ni shoga na kuvijuulisha vyombo husika baada ya kumuona kijana wa miaka 18 akiingia nyumbani kwa Padri huyo Jumatatu iliyopita.

Polisi imesema iliwakuta watu hao wawili wakiwa wamelala juu ya kitanda cha Padri na baada ya kuhojiwa wote wawili walikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja.

Mahusianao ya jinsia moja ni kinyume na sheria katika mataifa ya Afrika. Mashoga katika mataifa mengi wanakabiliwa na vitisho, na adhabu ya mahakama.

Sheria ya Kenya inapiga marufuku kitendo cha aina hiyo. Jirani yake Uganda ilipitisha sheria ya kifungo cha maisha kwa baadhi ya vitendo vya ushoga lakini mahakama ya katiba ya nchi hiyo ililipinga hilo.

No comments:

Post a Comment

Popular