Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa, kimeombwa kutoa msaada wa haraka kwa wakazi wa wilaya ya Chemba, ambao wamekumbwa na mafuriko yaliyosababisha kukosa makazi, baada ya nyumba zao kuathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Ombi hilo lilitolewa jana na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, katika ukumbi wa habari wa bunge mjini hapa.
Alisema mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa, zimeleta maafa makubwa kwa wakazi wa jimbo hilo, hivyo wanahitaji msaada wa haraka kunusuru maisha yao.
Nkamia alisema licha ya kutoa taarifa kwenye kitengo hicho, bado hakuna msaada wowote uliokwisha tolewa kwa wananchi.
"Kwa sasa wananchi wengi wamehamishiwa kwenye shule ya msingi Olboroti na shule ya Sekondari ya Kaloleni. Nimejaribu kuwasiliana na Ofisi ya maafa, lakini mpaka sasa hata kufika hawajafika. Jana (juzi), niliwasiliana na Waziri husika, ndio amesema atatuma mtu Alhamisi (leo).
"Tunahitaji msaada wa haraka ikiwemo chakula, mahema, dawa na vitu vingine muhimu kwa matumizi ya binadamu", alisema Nkamia.
Nkamia alisema kuwa, kutokana na mafuriko hayo, barabara ya Kondoa, Chemba hadi Kiteto, imeharibika vibaya na haiwezi kupitika kwa zaidi ya miezi sita.
"Mvua hii ni kubwa kwani maji yamejaa katika bwawa la Njiro na kumwagika kwenye maeneo ya mkazi", alisema.
Alisema mpaka sasa wanakijiji wa Kijiji cha Olboroti, kilichoko katika Kata ya Mrijo Chini, wamehamishwa wote kufuatia mafuriko hayo huku wakiwa hawana huduma yoyote.

No comments:
Post a Comment