Rais Magufuli afanya uteuzi TANESCO. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 17 January 2018

Rais Magufuli afanya uteuzi TANESCO.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli Jana  tarehe 17 Januari, 2018 amemteua Dkt Titus Mwinuka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kabla ya uteuzi huu Dkt Titus Mwinuka alikuwa akikaimu nafasi hiyo
Mnamo Januari 1, 2017 , Rais John Pombe Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba na kumteua Dkt Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo.

Kwa mwaka 2017 Mkurugenzi wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alikuwa mfanyakazi wa kwanza kutumbuliwa na Rais John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Popular