Mtei: Wingi wa benki nchini unahatarisha sekta ya fedha. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 9 January 2018

Mtei: Wingi wa benki nchini unahatarisha sekta ya fedha.

 
Aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Edwin Mtei ametahadharisha juu ya uwapo wa benki nyingi nchini akisema wingi wa taasisi hizo unaongeza hatari katika sekta ya fedha.

Mtei ambaye pia ni muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA alitoa kauli hiyo jana alipohojiwa kuhusu kufutiwa leseni ya biashara na kufungiwa kwa benki tano na tatu kuwekwa chini ya uangalizi.

“Kuzifuta baadhi ya taasisi ni mambo yanayotokea kwenye nchi zenye benki nyingi,” alisema Mtei.

No comments:

Post a Comment

Popular