Madiwani watatu wa CHADEMA wilayani Longido leo, Jumanne wamejivua gamba na kujiunga na CCM rasmi.
Madiwani hao ni pamoja na Jacob Mollel Silas wa Kata ya Elang’atadapash, Elias Mepukori Mbao wa wa Kata ya Kamwanga na Diyoo Lomayani wa Kata ya Olmolog .
Madiwani hao wamesema walitoka CCM mwaka 2015 baada ya kutotendewa haki kwenye kura za maoni na kutafuta haki nje ya CCM.
Akieleza sababu ya kurejea CCM, madiwani hao wamesema wamevutiwa na namna Rais John Magufuli anavyosimamia haki hususan haki za wanyonge na hivyo wameomba kurejea nyumbani ili washirikiane naye katika kujenga nchi.

No comments:
Post a Comment