Mitandao ya kijamii yamponza mkuu wa mkoa. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 9 January 2018

Mitandao ya kijamii yamponza mkuu wa mkoa.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe  Job Ndugai ameielekeza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kukutana ili kuchunguza na kujadili kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, inayodhalilisha Bunge.

Spika Ndugai amechukua hatua hiyo kufuatia kauli zilizonukuliwa katika mitandao ya kijamii kwa lugha za kimasai, Kiswahili na Kiingereza, zikiashiria kejeli na dharau kwa Bunge.

Ameelekeza kuwa wakati wa kuchunguza suala hilo Kamati imuite na kumuhoji ili kubaini ukweli na dhamira ya kauli hizo na kutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Bunge.

Hivi karibuni kulisikika sauti inayodaiwa kuwa ya Ole Sendeka ikizungumza kwa lugha ya kimasai iliyodaiwa kulisema Bunge na uongozi wake kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Bunge hilo.

No comments:

Post a Comment

Popular