Kijana asimulia jinsi alivyotupwa kwenye banda la mbwa, kisha mbwa mmoja kumuokoa. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 4 January 2018

Kijana asimulia jinsi alivyotupwa kwenye banda la mbwa, kisha mbwa mmoja kumuokoa.

 
 Kijana mmoja mwenyeji wa mkoani Singida ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kiwanda cha kutengenezea viatu vya yeboyebo  kilichopo Vikindu wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, ambapo mmiliki wa hicho kiwanda ni mtu mwenye asili ya China (Mchina).

Kwa mujibu wa kijana huyo anadai muajiri wake huyo mchina alimtupa kwenye banda la mbwa wanne ambao watatu ndio walimshambulia na yeye akawa anapambana nao.

Pia kijana huyo amesema akuweza kupata msaada wowote kutoka kwa binadamu kitu ambacho kilimfanya apate majehara sehemu mbalimbali za mwili wake na kuelekea kupasuka mdomo.

Kitendo hicho kilimchukiza Mmoja wa mbwa hao wanne alikuwa mbwa mkubwa ambaye hakumshambulia ila alipoona kijana ameanguka chini na hawezi kupambana tena na wale watatu ndipo alipowakoromea mbwa hao wengine watatu wakaacha kumshambulia kijana huyo.

Baadae ndiyo  wafanyakazi wengine wa kiwanda walikuja kumtoa kijana huyo kwenye banda hilo na kumpeleka  hospitali na aliweza kupata matibabu pia aliweza kushonwa mdomo aliopasuka.

Kutokana na kutokuwa na pesa za matibabu aliomba kutoka hospitalini na kwenda kujitibu mwenyewe nyumbani  lakini kutokana na uhaba wa fedha hajapona vizuri mpaka sasa.

Kisa cha muajiri huyo kufanya hivyo kwa mujibu wa kijana anasema alimwambia kuwa hawezi kufanya kazi katika kitengo ambacho alipangiwa kwa kua kulikuwa na moshi mkali ambao ulikuwa unaatalisha afya ya binadamu.

No comments:

Post a Comment

Popular