Mwanasiasa mkongwe Kingunge amefiwa na mke wake. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 4 January 2018

Mwanasiasa mkongwe Kingunge amefiwa na mke wake.

Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha taarifa hizo na kwamba kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

"Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling'atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka," amesema

No comments:

Post a Comment

Popular