Hatimaye serikali imemjibu Tundu Lissu. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 6 January 2018

Hatimaye serikali imemjibu Tundu Lissu.

 Serikali imesema haioni sababu ya kuendelea kulumbana na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu, ambaye, anapata matibabu jijini Nairobi baada ya kushambuliwa kwa risasi Mjini Dodoma takribani miezi minne iliyopita.

Msemaji Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan, Abbas, ametoa kauli hiyo kufuatia Mhe Lissu kuituhumu serikali juu ya kushambuliwa kwake na kumsababishia majeraha makubwa mwilinini mwake.
Dkt Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema, Mbunge huyo bado ni mgonjwa na kwamba Serikali inaendelea kumuombea Mhe Tundu Lissu ili apone haraka.

"Mhe Tundu  Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni busara kulumbana naye kwa sasa. Tunaendelea kumuombea apone haraka" ilisema taarifa ya Dkt Abbas

Tundu Lissu leo Januari 5, 2018 ametoa malalamiko yako na kusema kuwa kitendo cha yeye kupigwa risasi kuwa ni mipango iliyokuwa inalenga kumzimisha kabisaa ili asiendelee kuwasumbua.

No comments:

Post a Comment

Popular