Tundu Lissu asafirishwa kwenda nje ya bara la Afrika kwa matibabu zaidi. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 6 January 2018

Tundu Lissu asafirishwa kwenda nje ya bara la Afrika kwa matibabu zaidi.

 Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Mhe Tundu Antiphas Lissu ametoka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya leo asubuhi Jumamosi Januari 6, 2018. Kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi ya kuurejesha mwili wake katika hali yake ya kawaida.

Mhe Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanzania (TLS) ataondoka saa 2.30 asubuhi ya leo Jumamosi na ndege ya shirika la ndege la Kenya akiambatana na mke wake Alicia.

Mhe Lissu ametoka hospitalini hapo ukiwa baada ya matibabu aliyoyapata tangu Septemba 7 mwaka jana baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana kwenye makazi yake Dodoma.

Mwanasiasa huyo amesindikizwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa Jomo Kenyatta pia na watoto wake pacha, Augustino na Edward, Ndugu zake, viongozi na wanachama wa Chadema.

No comments:

Post a Comment

Popular