Polepole: Hatuna taarifa ya Wema Sepetu kurudi CCM. - KULUNZI FIKRA

Friday, 1 December 2017

Polepole: Hatuna taarifa ya Wema Sepetu kurudi CCM.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, ndugu Hamphrey Polepole amesema kuwa Chama hicho hakina taarifa yeyote ya kurudi kwa Wema Sepetu.

Akijibu swali kuhusu taarifa kuwa Wema amerudi CCM akitokea CHADEMA, ndugu Polepole amesema CCM ina utaratibu wa wanachama kujiunga na Chama hicho.

"Kupitia utaratibu na muundo wetu wa Chama cha Mapinduzi kwenye shina kisha ataandikwa kwenye orodha ya wanachama kwenye tawi ambalo yeye ni mkaazi", amesema ndugu Polepole.

No comments:

Post a Comment

Popular