TANESCO yatoa taarifa kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme nchini. - KULUNZI FIKRA

Friday, 1 December 2017

TANESCO yatoa taarifa kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme nchini.

 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa tamko juu ya katizo la umeme la siku ya pili mfululizo baada ya siku ya jana Novemba 30, 2017 shirika hilo kutangaza kuwa kutakuwa na katizo la umeme kwa watumiaji wa umeme wa gridi ya taifa kwa mikoa yote.

Katika hali ya kushangaza watu walijua katizo hilo ni la jana tu kama ilivyotangazwa lakini leo pia, Umeme umekatika ghafla na TANESCO tayari wametolea maelezo ya katizo hilo la umeme kwa siku ya pili kupitia kwenye tovuti yao taarifa hiyo imesomeka kama ifuatavyo.

Shirika la Umeme Tanzania linawataarifu Wateja wake kuwa wakati Wataalamu wetu wanaendelea kurekebisha mifumo yetu ya grid kutokana na hitilafu iliyotokea jana, Imegundulika mifumo ya Gridi haijatengemaa vizuri na hivyo wanaendelea na kazi kuhakikisha huduma ya umeme inarejea.

No comments:

Post a Comment

Popular