Joshua Nassari avamiwa na watu wenye bunduki nyumbani kwake. - KULUNZI FIKRA

Friday, 1 December 2017

Joshua Nassari avamiwa na watu wenye bunduki nyumbani kwake.

 
 Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amedai usiku wa kuamkia Jumamosi hii alivamiwa na watu wasiojulika wakiwa na bundiki na kufyetua risasi nje ya nyumba yake.

Nassari amedai muda mchache baada ya tukio hilo yeye pamoja na mke wake walifanikiwa kufika kituo cha polisi na kutoa ripoti na tukio hilo.

“Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu,” alitweet Joshua Nassari.

Amedai watu hao baada ya kufyetua risasi walifanikiwa kumuuwa mbwa wake ambaye alikuwa nje ya nyumba.

Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akiripoti katika mitandao ya kijamii kwa amekuwa atishiwa kuuawa mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Popular