Serikali kuwaburuza mahakamani watu wanaosema uongo. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 2 December 2017

Serikali kuwaburuza mahakamani watu wanaosema uongo.

 
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amewaonya baadhi ya watu wanaoendelea kutoa takwimu za uongo ambazo husababisha taifa kuingia kwenye mvutano na nchi wahisani wa maendeleo kwa kuogopa kusaidia wananchi.

Dkt. Chuwa amesema moja ya changamoto wanayokutana nayo katika ofisi yake na wadau wa maendeleo, ni baadhi ya takwimu kuonyesha ukubwa wa tatizo kwa kiwango ambacho hakijafikiwa, na kuleta hofu kwa wadau hao hali ambayo inasababisha taifa kukosa ushirikiano mzuri na nchi zingine, kwa kuogopa kusaidia taifa lenye nguvu kazi ya kusuasua.

Kutokana na hilo Mkurugenzi huyo anayesimamia masuala ya takwimu, ameagiza watendaji wake kuhakikisha wanawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kutoa takwimu za uongo, na kuliingiza taifa katika hali ya sintofahamu.

Kwa upande mwengine baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameiomba jamii kuacha kusambaza takwimu za uongo, na kuziachia mamlaka husika za serikali kutekeleza jukumu hilo la utoaji wa takwimu zilizosahihi.

No comments:

Post a Comment

Popular