Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea mjini na kata sita za Tanzania bara ambao utafanyika January 13 mwakani.
Akitoa taarifa kwa Umma jijini Dar es salaam jana Jumamosi Makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi (NEC) jaji mkuu mstaafu wa Zanzibar, Mhe Hamid Mohmaud Hamid amesema tume imetangaza ratiba ya uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa spika wa Bunge kwamba nafasi ziko wazi.
Jimbo la Singida Kaskazini liko wazi kutokana na kujivua uanachama wa chama cha mapinduzi CCM Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Lazaro Nyalandu, Songea mjini baada ya kifo cha Leonidas Gama na Jimbo la Longido baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yamempa ushindi Onesmo Ole Nangale.
Akizungumzia uchaguzi wa kata sita amesema waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa kwa kuzigatia masharti ya kifungu cha 13 (1) cha sheria ya uchaguzi ya Serikali za mitaa,sura ya 292 alitoa taarifa tume ya uchaguzi kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata hizo za Tanzania bara.
Alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandalu (Arusha), Kihesa (Iringa), Bukumbi (Uyui), Kurui (Kisarawe), Keza (Ngara), na Kwagunda (Korongwe).
Amesema utoaji wa fomu za uteuzi katika majimbo hayo na kata hizo sita utakuwa ni kati ya Desemba 12 na 18,2017 wakati katika jimbo la Songea mjini utoaji wa fomu utakuwa kati ya Desemba 14 hadi 20 mwaka huu.
Alifafanua kuwa kwa upande wa kampeni za uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata zote sita zitaanza Desemba 19 na kumalizika January 12 2018.
Katika jimbo la Songea mjini amesema kuwa kampeni zitaanza tarehe 21 Desemba 2017 na kumalizika tarehe 12 January 2018 wakati siku ya uchaguzi katika majimbo yote matatu na kata zote sita itakuwa tarehe 13 January 2018.
Jaji Hamid alivikumbusha vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi wazingatie sheria, kanuni taratibu, kiongozi na maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo wa majimbo hayo na kata zote sita.

No comments:
Post a Comment