Steven Nyerere amjia juu Polepole. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 2 December 2017

Steven Nyerere amjia juu Polepole.

 
 Gumzo la sasa hivi ni kuhusu Mwigizaji Wema Sepetu kutangaza kurudi kwenye Chama cha Mapinduzi CCM baada ya kukaa CHADEMA toka February mwaka 2017.

Baada ya Wema kutangaza huo uamuzi mpya, Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole alisema CCM haina taarifa za Wema Sepetu kurudi na hata hivyo watu huwa hawarudi kwenye Chama kupitia mitandao.

Kauli hiyo imewafanya Watu mbalimbali maarufu kutoa maoni yao akiwemo Steve Nyerere alieandika “hiki chama hujakiunda wewe wala kukianzisha wewe, umekikuta kama tulivyokikuta wote, kina waasisi wenye uchungu nacho na wako kimya“

“Wewe ni nani ukatishe watu moyo kukitumikia kama vile ndio unakimiliki, tulia polepole chama cha wote hiki, usilete ubinafsi kwenye kutumikia na kujenga ngome, hatuhitaji wenye cement na nondo tu, acha hata mwenye jiwe lake aweke kikubwa nyumba isimame, ni mchango pia," alisema  Steve Nyerere 

No comments:

Post a Comment

Popular