Mbunge wa Kinondoni atoa sababu za kujiuzulu na kujiunga na CCM. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 3 December 2017

Mbunge wa Kinondoni atoa sababu za kujiuzulu na kujiunga na CCM.

 
 Maulid Said Mtulia mbunge wa bunge la Tanzania kupitia Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CUF amejiuzulu uanachama na ubunge kupitia chama hicho kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Amesema mambo yote waliyoahidi tayari yanafanywa vizuri zaidi na CCM hivyo ni vigumu kuwa mpinzani.

Aidha ametanabaisha kuwa kwa sasa ili uwawakilishe wananchi vizuri inabidi uwe CCM kwani ndo kuna sera za kusaidia wananchi kwa sasa. Hivyo imekuwa ikimuwia vigumu kufanya kazi akiwa nje ya CCM.

"Mimi Maulid Said Abdallah Mtulia, mbunge wa jimbo  Kinondoni kwa tiketi ya Civic United Front (Cuf) chama cha wananchi kwa hiari yangu nimeamua kujiuzulu nafasi zangu zote za Uongozi nilizokuwa nashikilia ndani ya chama", amesema Mtulia.

" Nimefanya uamuzi huu tarehe 02/12/2017 kwa utashi wangu na bila shinikizo la mtu yeyote", amesema Mtulia.

"Sababu za kufanya hivi ni kutokana na uzoefu nilioupata kwa muda wa miaka miwili ya ubunge wangu ambapo nimebaini kuwa serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala kinafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na kimefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi upinzani tuliahidi kuyatekeleza", amesema Mtulia.

" Kwa kuwa nia yangu ni kuwatumikia wananchi, sioni sababu ya kuendelea kuwa upinzani na badala yake nimeona ni vema niungane na juhudi za serikali kwa kumuunga mkono Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo na kukabiliana na kero mbalimbali",amesema Mtulia.

Nawashukuru sana wananchi wa jimbo la Kinondoni kwa kunipm dhamana ya kuwa Mbunge katika uchaguzi mkuu uliopita na nawahidi kuwa nipo tayari kuendelea kushirikiana nanyi katika maendeleo nikiwa katika uwanja mwingine wa siasa ambao ni chama cha mapinduzi (CCM)", amesema Mtulia.

"Pia niwaombe wananchi na viongozi wengine ambao wanatambua mchango wa Mhe Rais Magufuli na serikali yake kutosita kuungana nae katika kazi za kuitumikia nchi badala ya kuwa wapinzani", amesema Mtulia.




No comments:

Post a Comment

Popular