Watu 34 wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi huku matukio 67 ya ukatili huo yakiripotiwa kwa kipindi cha miaka 11 katika maeneo mbalimbali nchini mkoa wa Mwanza ukiwa kinara kwa kuwa na kesi 15.
Takwimu hizo zinatolewa katika muendelezo wa mkakati wa kitaifa wa kupiga vita ukatili mauaji na unyanyasaji walemavu wa ngozi ambapo wakili kutoka Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka Bi Beatrice Isembo anasema mbali na adhabu hizo za vifo watuhumiwa wengine 17 wamehukumiwa vifungo tofauti na kesi zingine zikiendelea.
Ralph Meela ni Mrakibu Muandamizi wa Polisi kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi Idara ya Upelelezi Kitengo cha Makosa dhidi ya binadamu na usalama barabarani anasema asilimia kubwa ya mauaji hayo yanatokana na imani za kishirikina huku maeneo yaliyoathirika zaidi ni sehemu za migodi na uvuvi hasa kwenye ziwa victoria
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu nchini Bahame Nyanduga anasema mauaji na ukatili kwa watu walemavu wa ngozi ni suala la kupigwa vita na jamii yote huku Bi Prepetua Sinkolo Afisa Utetezi wa Haki za binadamu akisema elimu inahitajika miongoni mwa jamii hata katika maeneo ambayo matukio hayo hayajaripotiwa kujitokeza.
Mkakati huo wa kitaifa unaratibiwa na chini ya mwamvuli wa Tume ya haki za binadamu kwa kushirikiana na Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Mkurugenzi wa Mashtaka serikali na asasi za kiraia ambao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa kupunguza tatizo hilo.

No comments:
Post a Comment