Wabunge wa chadema wazidi kusota Mahabusu. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 30 November 2017

Wabunge wa chadema wazidi kusota Mahabusu.

 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, imewanyima dhamana, Wabunge Peter Lijualikali, Suzan Kiwanga na wafuasi wengine 34 wa Chadema wakiwepo madiwani, na kuwarudisha mahabusu hadi Disemba 04 mwaka huu.

Wabunge hao walikamatwa mapema wiki hii kwa tuhuma za kufanya vurugu katika uchaguzi wa madiwani ikiwa ni pamoja na kuchoma shule na rasilimali nyingine za umma.

Mapema wiki hii Polisi wa mkoani Morogoro inawatia mbaroni watu 41 akiwemo mbunge wa Mlimba (Chadema), Susan Kiwanga, madiwani wawili kwa madai ya  kufanya fujo na kuchoma moto majengo ya shule baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Sofi

Kamanda wa Polisi Ulrch Matei alisema kwambaViongozi hao walikuwa wakiwachochea wafuasi wa chama hicho kuchoma moto  nyumba ya walimu wa shule ya Sofi na ofisi ya mtendaji kata na pia hataa baada ya kuchoma majengo hayo kwa kutumia petroli, walidhamiria pia kwenda katika zahanati lakini askari waliwakamata.

Mbunge Lijualikali yeye alijisalimisha baada ya kupata taarifa kwamba anatafutwa.

No comments:

Post a Comment

Popular