Msando: Sijawahi kumzungumzia Zitto kabwe toka nimeamia CCM. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 30 November 2017

Msando: Sijawahi kumzungumzia Zitto kabwe toka nimeamia CCM.

Mwanasheria maarufu wa Tanzania Alberto Msando amehojiwa leo kwenye 360 ya CloudsTV na kuzungumzia ishu mbalimbali ikiwemo kuhamia CCM, mpango wa kugombea Ubunge, video yake na Gigi Money na mengine.

Msando ambae alikua ACT Wazalendo kabla ya kujiunga na CCM juzi, ameeleza kuwa amejiunga CCM na anaunga mkono kile anachokiongoza na kukisimamia Rais John Magufuli katika chama hicho na kwa wale wanaomuita Msaliti ameongea yafuatayo hapa chini.

Amesema hii sio mara ya kwanza yeye kuhama chama hivyo kwa sasa ingebidi waseme amerudi nyumbani, chama ambacho alikuwepo kabla ya kuhama mara ya kwanza na hajahamia CCM ili agombee Ubunge Arusha lakini ifahamike kuwa akigombea atagombea ili ashinde na sio kujaribu.

“Kuwepo kwangu kwenye siasa hakukuanza Jumanne ambayo ndio nilijiunga na Chama cha Mapinduzi ambacho ndio Chama changu na niseme sasa ndio tunatumia msemo Chama pendwa, Chama tawala, nimekuwepo kwenye siasa kwa muda mrefu” – Albert

“Kuhusu video na Giggy sikuwa namfahamu na kusema kweli tukio lile lilitokea wakati nimekunywa pombe, hata hivyo ile video ilinisaidia kujua jamii inanichukuliaje na nini inategemea kutoka kwangu, sikuwa namfahamu Giggy na hata juzi nilikutana nae kwenye ndege sikumkumbuka.

“Niliacha kuwa Wakili wa Wema Sepetu baada ya Kibatala na Lissu kuanza kumtetea, bado ni mshikaji wangu, na nimekua nikiona hiyo habari inayozunguka kuhusu Wema Sepetu kujiandaa kurudi CCM, namkaribisha”

“Kuna watu wanashindwa kuelewa kwamba Asilimia 90 kwenye hizi kamatakamata, majina makubwa ya wanaokamatwa kwenye kesi za ufisadi, utakatishaji fedha na nyingine ni Watu wa CCM, Rais Magufuli anafanya kazi“

Ushindi wa CCM kwenye uchaguzi wa Udiwani kata 42 wanastahili, ni maamuzi ya Wananchi baada ya kuona kazi iliyofanywa na Serikali kwenye hii miaka miwili, hamna watu ni wepesi kugeuka kama Wapiga kura… huu ushindi wa juzi ni ushindi ambao CCM walistahili, Rais ameshaonyesha njia na Wananchi wameona.

Mimi ni Albert Msando ni Mwanasheria na nitaendelea kubaki Mwanasheria… ni Mwanasheria ambae nitatumia utaalamu wangu wa Sheria katika siasa kusaidia wengine.

Kuhusu kumsaliti Zitto Kabwe na kuihama ACT WAZALENDO, Msando amesema “nikiri kwamba sijazungumza na Zitto toka nimehama ACT wala sikumpa taarifa, sina tatizo nae na hata jina la Mtoto wake wa kwanza ni mimi nilimpa, hata nilipotoka CHADEMA nilikaa mwaka mzima bila kuzungumza na Mbowe lakini baadae alielewa na maisha yakaendelea”

No comments:

Post a Comment

Popular