Katibu wa chadema wahamia CCM. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 29 November 2017

Katibu wa chadema wahamia CCM.

 Katibu wa CHADEMA wilayani Simanjiro, mkoa wa Manyara, Meshack Turento ametangaza kujivua wadhifa huo na kujiunga na chama cha mapinduzi akidai CHADEMA imewatelekeza.

Akizungumza jijini Arusha alidai kuwa kabla ya kujiunga na CHADEMA alikuwa mwanachana wa CCM, lakini baadae aliona chama hicho kimepoteza mwelekeo na kujiunga na CHADEMA, ila sasa ameamua kurejea CCM baada ya kuona ndani ya CCM kuna mabadiliko makubwa.

Pia alisema kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wa rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM taifa kwa kuimarisha chama hicho na kukijengea Mfuko mzuri wa madaraka

Hata hivyo alikanusha taarifa za yeye kutishwa kukamatiwà mifugo yake iwapo ataendelea kubaki CHADEMA na kudai si za kweli na wala hajanunuliwa.

No comments:

Post a Comment

Popular