Mkuu wa mkoa wa Morogoro anusurika katika ajali mbaya. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 29 November 2017

Mkuu wa mkoa wa Morogoro anusurika katika ajali mbaya.

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt Steven Kebwe amepata ajali katikati ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo wilayani Kilosa mkoani hapa.

Ajali hiyo ilitokea saa saba usiku wa kuamkia Juzi  Jumatano ambapo inadaiwa gari la mkuu huyo wa mkoa lilimgonga mnyama aina ya Nyati na gari hilo kuharibika vibaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa taarifa kamili ataitoa mara baada ya kukamilika.

Inadaiwa kuwa ndani ya gari hilo mbali na kuwepo mkuu wa mkoa pia aliambatana na mlinzi wake ambao wote kwa pamoja walitoka salama.

Mwandishi wa kulunzifikra blog  ilifanya juhudi za kumtafuta mkuu wa mkoa kwa njia ya simu ili kuzungumza naye juu ya ajali hiyo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

No comments:

Post a Comment

Popular