Serikali imeshauriwa kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa kwa kuzijengea uwezo taasisi zake na kuboresha sheria ili kuongeza uwazi na uwajibikaji wa viongozi katika rasilimali muhimu za taifa.
Akizungumza Jana jijini Dar es Salaam katika Mdahalo wa Demokrasia uliondaliwa na Twaweza, Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe Zitto Kabwe amesema serikali imepiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa lakini inapaswa kujiendesha kwa uwazi na kuruhusu taasisi zake kuwajibika katika manunuzi na matumizi ya fedha za umma.
“ Moja ya jambo ambalo linaisaidia sana serikali kukabiliana na ufisadi ni uwazi kwa sababu inatoa uhuru wa wananchi kutoa taarifa na kuweza kuzifanyia kazi”, amesema Mhe Zitto kabwe
Mhe Zitto kabwe ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo amesema usiri wa serikali unawanyima wananchi haki ya kupata taarifa muhimu za miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa mfumo wa uwazi na uwajibikaji unaanzia kwenye taasisi ambazo zimewekwa kisheria kusimamia rasilimali za nchi zikiwemo Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Kamati za Bunge kufanya kazi kwa uhuru na kutoa mapendekezo yao juu ya uboreshaji wa changamoto zilizopo katika jamii.
“ Taasisi za uwajibikaji kama Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kamati muhimu za Bunge za Mahesabu kama hazina uwezo wa kufanya shughuli zao kwa uwazi na uhuru maana yake kwamba baada ya awamu hii kutoka na kumaliza muda wake tutakuwa na kazi ngumu sana ya kupambana na madhira ya ufisadi kama ambavyo yanavyoshughulikiwa sasa hivi”, amesema Mhe Zitto kabwe.
Amesema serikali ya awamu ya nne ilijitahidi kuimarisha taasisi zake za uwazi na uwajibikaji ambazo ziliibua ufisadi mkubwa kama Tegeta Escrow, Richmond, Meremeta ambao uliligharimu taifa mabilioni ya fedha. Ameitaka serikali kuendeleza utamaduni huo na kuondoa dhana ya usiri katika uendeshaji wa shughuli zake.
“Wito wangu ni lazima kuondeleza zile juhudi za uwazi na ujenzi wa taasisi ambao umeanza ili taasisi ziendelee kuwa huru kwa ajili ya nkuweza kuibua mambo kama haya”, ameshauri Mhe Zitto kabwe
Hata hivyo, Mhe Zitto kabwe ameitaka Ofisi ya CAG na PPRA kuchunguza fedha zilizotumika kujenga uwanja wa ndege wa Chato, ambao haujafuata taratibu za kisheria na haukupitishwa na bunge, ili wananchi wapate taarifa za uhakika na kuondoa mjadala ambao haujapatiwa majibu ya uhakika kutoka serikalini
Ikumbukwe kuwa katika kikao cha tisa cha Bunge, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche aliibua sakata la ujenzi wa uwanja huo lakini majibu ya uhakika hayakutolewa. Uwanja huo ambao unadhaniwa kugharimu zaidi za bilioni 39 unajengwa katika mji wa Chato anakotoka rais John Magufuli.
“Si vibaya kujenga viwanja vya ndege na Chato ni Tanzania kama sehemu nyingine yoyote ya Tanzania na hatuwezi kutopenda wenzetu kupata maendeleo lakini jambo la muhimu ni namna gani ule mradi unatekelezwa haukuwa kwenye mipango ya bajeti, hapakuwa na zabuni ya wazi”, amesema Mhe Zitto kabwe na kuongeza kuwa,
“Kampuni ambayo imepewa kufanya ile kazi haijawahi kujenga kiwanja chochote cha ndege, katika mazingira kama haya uwazi ungeweza kusaidia kwa sababu PPRA ambayo ni mamlaka ya manunuzi ya umma ingeweza kufanya uchunguzi na kuweza kutueleza uhalisia wa jambo hili. Kwa sababu ni fedha nyingi zinatumika pale, zaidi ya bilioni 39”.

No comments:
Post a Comment