Halima Mdee amkaribisha Lazaro Nyalandu kwa tahadhari kubwa - KULUNZI FIKRA

Monday, 30 October 2017

Halima Mdee amkaribisha Lazaro Nyalandu kwa tahadhari kubwa

Mbunge wa jimbo la Kawe, Mhe. Halima Mdee amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Mhe Lazaro Nyalandu ndani ya CHADEMA kwa kumtahadharisha kuhusu changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa vyama vya upinzani.

Halima Mdee ametoa tahadhari hizo mapema Jana baada ya Mhe Nyalandu kutangaza kujiuzulu nafasi yake zake za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kujivua ubunge.

“Mhe. Nyalandu karibu sana CHADEMA naamini utakuwa imara kukabiriana na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabiri Taifa letu.“ameandika Mhe. Mdee kwenye ukurasa wake wa Twitter na kumtahadharisha Lazaro  Nyalandu

“Mhe. Lazaro Nyalandu nikukaribishe kwenye siasa za upinzani Tanzania! ni siasa tamu sana kwa wenye moyo mgumu! Ni ngumu sana kwa wenye moyo mwepesi.”

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe Freeman Mbowe nae amemkaribisha Nyalandu kwa kumwambia kuwa milango iko wazi.

“Milango iko wazi kwako @LazaroNyalandu kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu.“ameandika Mhe. Mbowe kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mapema Jana Mhe. Lazaro  Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM ametangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kutokufurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuomba nafasi ya kujiunga na CHADEMA kama wataridhia ili kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini.

No comments:

Post a Comment

Popular