Wagonjwa wa akili waongezeka Tanzania - KULUNZI FIKRA

Tuesday 5 September 2017

Wagonjwa wa akili waongezeka Tanzania

Tafiti zilizotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zinaonyesha kuwa magonjwa ya akili yameongezeka kutoka wagonjwa laki 6 mwaka 2014-2015 hadi wagonjwa laki 7 kwa mwaka 2015-2016.

Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika wizara ya afya Bw. Shadrack Buswelu.

Takwimu hizo zimetolewa na Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika wizara ya afya Bw. Shadrack Buswelu kwenye mafunzo kwa watumishi wa magereza na hospitali za mikoa na kusema kinachochangia ongezeko la ugonjwa wa akili kuongezeka nchini ni mfumo wa maisha ulivyo kwa sasa, magonjwa sugu na matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake Mratibu wa Magereza SP Wambili Bwatai amesema tatizo la magonjwa ya akili gerezani ni mara mbili ya wagonjwa waliopo nje na wao kwa kuliona hilo wameamua kutoa mafunzo kwa maafisa hao ili kupunguza tatizo hilo kwa watu wanaotumikia kifungo.

No comments:

Post a Comment

Popular