Simba, Yanga uso kwa uso oktoba 28 - KULUNZI FIKRA

Tuesday 5 September 2017

Simba, Yanga uso kwa uso oktoba 28

 WAKATI benchi la ufundi Simba likifurahia kuona viungo wake wakifunga mabao, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limelitangaza ratiba mpya ambapo pambano la watani, Simba na Yanga sasa litapigwa Oktoba 28 Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam badala ya Oktoba 14.

Katika mabadiliko hayo mechi zilizopagwa zichezwe kesho Jumatano sasa zitachezwa wikiendi huku pambano la marudiano la watani litasubiri ya hatma ya timu hizo katika michuano ya kimataifa japo inaonyesha zitacheza Machi 14 mwakani.

Msimu huu Simba imepiga hesabu kali ambazo pengine zitawaacha midomo wazi Yanga.

Simba ilifanya tathmini na kugundua ikibaki tu kuwategemea mastraika, haitaweza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara, hivyo ikaweka nguvu pia katika eneo la kiungo.

Washindi hao wa Kombe la FA wameanza kuipoteza Yanga kwa kuwekeza katika eneo hilo ambapo viungo wake wanajua kuzifumania nyavu tofauti na Yanga inayowategemea zaidi mastraika; Amissi Tambwe, Ibrahim Ajibu, Obrey Chirwa na Donald Ngoma.

Simba licha ya kuwa na mastraika watatu; Juma Liuzio, Nicholas Gyan na Laudit Mavugo, imeweka nguvu kwa mawinga na viungo ambao wakiingia kwenye boksi tu umelia.

Viungo hao wanaofanya vizuri ni Mohammed Ibrahim, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla na Emmanuel Okwi anayemudu pia kucheza straika.

No comments:

Post a Comment

Popular