Kambi ya Upinzani Bunge wasusia kuapishwa kwa wabunge wapya wa cuf - KULUNZI FIKRA

Tuesday 5 September 2017

Kambi ya Upinzani Bunge wasusia kuapishwa kwa wabunge wapya wa cuf

Kambi rasmi ya upinzani Bungeni imesusia kuapishwa kwa wabunge saba wa viti maalum kutoka chama cha Cuf.

Wabunge hao wameapishwa leo septemba 5 na spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Wakati wabunge hao wakitoka ndani ya ukumbi wa Bunge,baadhi ya wabunge walibaki kushuhudia wabunge wa Cuf wakiapishwa wabunge waliobaki kutoka mambo rasmi ya  upinzani ni Magdalena Sakaya (Kaliua),  Maftah Nachuma (Mtwara mjini) na Maulid Mtulia ( kinondoni)

Awali, wafuasi wa Cuf walifika asubuhi katika viwanja vya Bunge kushuhudia kuapishwa kwa wabunge hao walioteuliwa hivi karibuni na Tume ya Taifa uchaguzi ( NEC).

Wafuasi hao waliambatana na Mbunge wa Bunge la Afrika mashariki, Habibu Mnyaa walifika wakiwa kwenye magari matatu aina ya Toyota coaster na mengine madogo yaliyokuwa yamebandikwa licha za mwenyekiti wa wa Cuf, Ibrahimu Lipumba anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini.

Wabunge wa viti maalum walioapishwa leo ni Alfredina Kiangi, Kiza Mayeye, Huru Bafadhili ,Rukia Kassima, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.

Hindu Mwenda ambaye angeapishwa leo alifariki dunia ijumaa ya septemba  mosi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa jumapili ya septemba 3.

No comments:

Post a Comment

Popular