Mbwana Samatta ajitetea kwa kutozifumania nyavu kwenye mechi ya Jana. - KULUNZI FIKRA

Sunday 3 September 2017

Mbwana Samatta ajitetea kwa kutozifumania nyavu kwenye mechi ya Jana.

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kitendo cha yeye kutofunga bao katika mchezo dhidi ya Botswana siyo cha kushangaza kwa kuwa timu ina wachezaji 11 na kinachohitajika ni ushirikiano wa pamoja.

Samatta alisema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 2-0 yote yakifungwa na Simon Msuva.

Katika mchezo huo Samatta alionekana kutocheza katika kiwango chake kilichozoeleka na hivyo kuwapa hofu baadhi ya mashabiki waliohudhuria mchezo huo.

“Hii ndiyo maana ikaitwa timu, siyo lazima Samatta afunge, akifunga mwingine au mimi nikicheza chini ya kiwango huku timu ikipata ushindi yote ni sawa, siku hazifanani lakini kwa ufupi timu yetu ilikuwa na uwezo mzuri kuliko wao (Botswana),” alisema Samatta ambaye ni mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji.

Naye Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema amefurahishwa na wachezaji ambao amewaita kwa mara ya kwanza katika kikosi hicho na kuahidi kuzidi kuwapa nafasi wengine ambao hajawahi kuwaita.

Ushindi huo wa Taifa Stars ni wa sita kwa Mayanga tangu akabidhiwe mikoba ya kukinoa kikosi hicho kutokea kwa Charles Boniface Mkwassa ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Yanga.

Lakini, Mayanga ameiongoza Taifa Stars kucheza mechi 12, ambazo sita akishinda, tano akitoka sare na kufungwa mechi moja.

Kwa upande wa kocha mkuu wa Botswana 'The Zebras', David Bright amemwagia sifa kipa wa Stars, Aishi Manula ambaye alionekana kuwa kizingiti kikubwa cha wao kukosa matokeo chanya

No comments:

Post a Comment

Popular