Kapombe aongezewa muda wa matibabu - KULUNZI FIKRA

Sunday, 3 September 2017

Kapombe aongezewa muda wa matibabu

Pamoja na daktari kumuongezea wiki mbili zaidi za matibabu, huenda beki Shomari Kapombe atarajea mapema dimbani.

Kapombe ambaye anasumbuliwa na nyonga, aliongezewa wiki mbili za kupata matibabu.

Lakini taarifa kutoka Simba zinaeleza huenda beki huyo akarejea mapema kama kutakuwa na maendeleo mazuri.

“Kweli ni wiki mbili lakini daktari anachofanya ni kuangalia hali inavyokwenda. Kama nafuu itakuwa imepatikana haraka, basi anaweza kuanza kujifua taratibu.

“Unajua Simba wana bahati moja, wana daktari lakini hata meneja wao ni daktari. Hivyo kwa afya za wachezaji si jambo la hofu kwao,” kilieleza chanzo.

Kapombe amerejea Simba akitokea Azam FC aliyojiunga nayo akitokea AS Cannes ya Ufaransa. Hata hivyo, bado haijaichezea Simba kutokana na kuandamwa na maumivu hayo ya nyonga.

No comments:

Post a Comment

Popular