Waziri mkuu Kassimu Majaliwa atoa suluhisho la ajira nchini - KULUNZI FIKRA

Sunday, 3 September 2017

Waziri mkuu Kassimu Majaliwa atoa suluhisho la ajira nchini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda katika maeneo yao kwani  vitasaidia katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana.

Waziri Mkuu alipozungumza na watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro amesema mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda ambao unalenga kuinua uchumi wa Taifa kutoka wa chini kwenda uchumi wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia.

“Viwanda hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa vijana kwa sababu vinauwezo wa kuajiri watu wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji wake. Lakini mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda vitawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya kilimo kuwa na tija,"amesema  Mhe. Majaliwa.

Pamoja na hayo Majaliwa ameongeza na kusema kwamba muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo ambalo lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa soko.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesisitiza uaminifu kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda mbalimbali kuwa waaminifu ili kuviwezesha viwanda hivyo kuendelea na uzalishaji.

No comments:

Post a Comment

Popular