Mbunge mpya wa Cuf, Bi Hindu Mwenda afariki dunia - KULUNZI FIKRA

Saturday, 2 September 2017

Mbunge mpya wa Cuf, Bi Hindu Mwenda afariki dunia

 Mmoja kati ya wabunge 8 wateule kutoka Chama cha Wananchi CUF Bi. Hindu Hamis Mwenda amefariki dunia.

Taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa chama hicho Abdul Kambaya imesema kuwa Bi Hindu amefariki katika hospitali ya taifa Muhimbili jana jioni alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Taarifa hiyo haijaeleza kwa undani chanzo cha kifo hicho, lakini amesema taratibu nyingine zinazofuata zitaelezwa baadaye.

Wabunge hao wapya wa viti maalum pamoja na marehemu, waliteuliwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada waliokuwa wakishika nafasi hizo kuvuliwa ubunge kutokana na kuvuliwa uanachama na hivyo kupoteza sifa ya kuwa wabunge.

Mwanzoni mwa wiki hii Spika wa Bunge Job Ndugai alitamka kuwa wabunge hao wapya wataapishwa katika kikao cha kwanza cha mkutano ujao wa bunge utakaoanza Septemba 5 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Popular