Mbatia ahoji kama kweli chadema inaamini katika ukawa - KULUNZI FIKRA

Saturday, 2 September 2017

Mbatia ahoji kama kweli chadema inaamini katika ukawa

 Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amehoji kuhusu hatua ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutaka kuwaadhibu madiwani sita wa CHADEMA waliompigia kura mgombea wa NCCR-Mageuzi katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo ndugu Filbert Shayo wa NCCR-Mageuzi aliibuka mshindi baada ya kumbwaga Deogratius Mushi wa CHADEMA.

"Je, ni ukweli wenzetu wa CHADEMA bado wana nia ya dhati ya dhana ya UKAWA? Ati leo Mbowe anashangazwa na ushindi wa mgombea wa NCCR-Mageuzi licha ya CHADEMA kuwa na wingi wa madiwani?
Kwahiyo Freeman anahoji kitendo cha madiwani hao kumpigia kura mgombea anayetokana na NCCR na kukitafsiri kuwa ni usaliti dhidi ya CHADEMA?

 Mbona amekaa kimya kuhusu madiwani wa CHADEMA waliompigia kura Mwenyekiti wa kamati ambaye anatoka CCM?" amehoji kwa mshangao James Mbatia.

Juzi, uongozi wa CHADEMA Wilaya ya Moshi Vijijini uliwaandikia barua madiwani hao, ukiwapa wiki mbili kujieleza kwa nini wasiadhibiwe kwa kumpigia kura mgombea wa NCCR-Mageuzi, Filbert Shayo.
    

No comments:

Post a Comment

Popular