Klabu ya Simba yanena juu ya Nicholas Gyan. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 2 September 2017

Klabu ya Simba yanena juu ya Nicholas Gyan.

 
 Klabu ya Simba imefunguka na kuweka sawa kuwa straika wao mpya raia wa Ghana, Nicholas Gyan ametua nchini Tanzania na kujiunga rasmi na klabu hiyo ambayo kwa sasa ndiyo klabu inayoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara 2017/2018.

Nicholas Gyan ni kati ya wachezaji ambao walikipiga siku ya Simba Day Agosti 8, 2017 ambapo Simba SC ilicheza game ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda katika uwanja wa Taifa Dar es salaam ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

"Baada ya kusajiliwa na kucheza kwenye siku ya Simba Day kisha kurudi Ghana kumalizia utaratibu, Nicholas Gyan amewasili rasmi kuitumikia Simba Sc. Ikumbukwe kuwa Nicholas alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Ghana. Karibu sana Nicholas Simba Sc" ilisema taarifa ya Simba

No comments:

Post a Comment

Popular