Kenyatta ang'aka juu hoja ya tume mpya ya uchaguzi - KULUNZI FIKRA

Saturday, 2 September 2017

Kenyatta ang'aka juu hoja ya tume mpya ya uchaguzi

 
 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema chama chake ambacho ni muungano wa Jubilee wamekubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Juu nchini humo, lakini hawapo tayari kukubali hoja ya upinzani inayotaka kubadili uongozi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Rais Kenyatta amesema hayo leo Jumamosi Septemba 2, alipozungumza na wabunge na maseneta ambao wameshinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 8, mwaka huu kupitia muungano wa Jubilee.

“Wacha niwaambie, tumekuwa hapa kabla, wameitimua IEBC yote ya zamani, kama wanafikiri, hatuna muda huo, kama wamekubali matokeo yote yaliyosalia, tukubali maamuzi ya mahakama” alisema kiongozi huyo.

“Lakini msiingilie na msifikirie kwamba kwa sababu rafiki zetu wamepiga kelele na sisi tumenyamaza kimya eti kwamba tunawaogopa, hapana” aliongeza Kenyatta.

Jana Ijumaa Mahakama ya Juu nchini Kenya, ilifuta matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita na kuamuru kufanyika kwa uchaguzi wa marudio, baada ya siku 60.

Uamuzi huo wa mahakama ulipokelewa kwa shangwe na muungano wa vyama vya upinzani (NASA) na kudai kutokuwa na imani tena na uongozi wa tume hiyo.

No comments:

Post a Comment

Popular