Majaji nchini Kenya wamjia juu Kenyatta - KULUNZI FIKRA

Sunday, 3 September 2017

Majaji nchini Kenya wamjia juu Kenyatta

Chama cha mawakili nchini Kenya ( LSK) kimemkosoa Rais Uhuru Kenyatta, baada ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi wa kubatilisha matokeo uchaguzi nchini Kenya.

Rais wa LSK Isaac Okero alimkosoa Rais Kenyatta kwa kumtaja jaji mkuu, David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa wamekosea.
Rais Kenyatta ametoa matamshi hayo wakati wa ziara ya kukutana na wasuasi wake katika soko la Burma mjini Nairoba,baada ya Mahakama hiyo ikiongozwa na jaji Maraga kufuta matokeo ya uchaguzi wa Rais.

Okero amesema matamshi ya kwamba majaji hao wasubiri Rais achaguliwe katika uchaguzi ujao hayafai kutoka kwa kiongozi wa taifa ambaye chini ya katiba ya Kenya ni nembo ya umoja wa wa Kenya.

No comments:

Post a Comment

Popular