Harouna Niyonzima afunguka kinachombakisha Tanzania - KULUNZI FIKRA

Friday 1 September 2017

Harouna Niyonzima afunguka kinachombakisha Tanzania

Mashabiki wengi wa soka Tanzania wanaamini kiungo ,Harouna Niyonzima, amekomaa Tanzania kwa kuwa anavuna fedha nyingi,lakini mwenyewe amefunguka kuwa mazingira rafiki ya kuishi na kufanya kazi ndiyo hasa yanamfanya asitamani kuondoka.
Niyonzima ambaye ni raia wa Rwanda,amedumu katika ligi kuu Tanzania bars kwa miaka sita,baada ya kusajiliwa kwa Mara ya kwanza na Yanga mwaka 2011 akitokea APR ya nchini kwao.
Baada ya kujiunga na Yanga, kiungo huyo aliichezea kwa miaka mitano na kuisaidia kushindwa taji la ligi kuu bars Mara nne, kabla ya msimu uliopita kuikacha na kujiunga na simba.
Usajili wake simba ulizua sokomoko miongoni mwa mashabiki wa Yanga, ambao baadhi walichukua uwamuzi wa kuichoma jezi namba nane iliyokuwa inatumiwa na kiungo huyo wakati anaitumikia timu hiyo.
Akizungumza na kulunzifikra blog Niyonzima alisema amani iliyoko Tanzania na upendo walionao wananchi wake vimekuwa vikimfanya ahisi kama yuko nyumbani kwao Rwanda.
"Nilipata ofa nyingi nje ya Tanzania kwaajili ya kwenda kucheza soka lakini sikutaka kwenda kwa kuwa hapa ninaishi vizuri sana na familia yangu.
" Nikitaka kwenda nyumbani na kwenda na kurudi vizuri, jambo hiki limenifanya nishindwe kabisa kuihacha hii nchi,"alisema Niyonzima.
Niyonzima alisema mpango wake ni kuhakikisha unaendelea kuishi Tanzania hata baada ya kutundika daluga.
"Mafanikio mengi ya soka nimeyapata nikiwa hapa, sikwamba mimi ndiye mchezaji nzuri kuliko wote, hapana, wapi wengi zaidi yangu yangu, lakini ni Mungu ndiye anapanga yote.
" Nimepanga hata baada ya kuachana na soka niendelee kubaki hapa, kwani Tanzania ni nchi ya pili baada ya Rwanda nilikozaliwa",alisema Niyonzima.
Ukiachilia sababu hizo,kiungo huyo inadaiwa ana uswahiba na Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga, Abdallah Bin Kleb ambaye alifanikisha usajili wake katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Popular