Geita: polisi wapiga marufuku kongamano la Chadema. - KULUNZI FIKRA

Sunday 3 September 2017

Geita: polisi wapiga marufuku kongamano la Chadema.

Kwa mara nyingine tena jeshi la polisi mkoani Geita limepiga marufuku, kongamano la kuadhimisha miaka 25 ya CHADEMA lililopangwa kufanyika leo tarehe 03/09/2017 ambalo maandalizi yake yamekamilika.

Sababu zilizotolewa na mkuu wa polisi wilaya ya Geita, SSP Ally Kitumbi ni kwamba hakuna polisi wa kutosha kwa ajili ya kulinda kongamano hilo kwa kuwa polisi wapo kwenye maandalizi ya usimamizi mtihani wa darasa la saba.

Ikumbukwe kwamba polisi walizuia kongamano hili kwa mara ya kwanza tarehe 06/08/2017 kwa maelezo kuwa jeshi la Polisi lilikua katika maandalizi ya kupokea mwenge wa uhuru, na hivyo wakakosa askari wa kutosha wa kulinda kongamano hilo. Leo tena polisi wanasema hawana askari wa kutosha kulinda kongamano hilo kwa kuwa wapo kwenye maandalizi ya mtihani wa darasa la saba.

Kutokana na polisi kila mara kudai hakuna askari wa kutosha, Chadema wameomba ruhusa ya kufanya kongamano hilo bila ulinzi wa Polisi kwa kuwa maandalizi yote yamekamilika, lakini polisi wamekataa.

No comments:

Post a Comment

Popular