Hali ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam imewaibua baadhi ya wabunge ambao wamesema ni mbaya, jambo linalotia aibu.
Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), Ali Salim Khamis amesema katika jengo la abiria paa linavuja na kuna joto kali.
“Naweza nikapata shaka iwapo Terminal III nayo kwa miaka saba inaweza ikaanza kuvuja, Uwanja wa Julius Nyerere kwa kweli unatuaibisha,” amesema.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana Agosti 29, wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (Pac) ilipokutana na Mamlaka vya Viwanja vya Ndege Tanzania (Taa).
Amesema Taa ina viwanja vingi vya ndege lakini vinavyochangia mapato ni vichache, huku vingine vikiwa havifanyi kazi.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Munde Tambwe amewataka wabunge waisaidie mamlaka hiyo ipate fedha za kutosha ili kuboresha viwanja vya ndege nchini.
“Kwa kweli ni aibu uwanja wa ndege Dar es Salaam. Tuwasaidie ili waweze kuongezewa fedha,” amesema.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Pac, Naghenjwa Kaboyoka amesema hali katika uwanja huo ni aibu lakini Serikali badala ya kuukarabati inajenga viwanja vingine, kikiwemo cha Chato.
Amesema kuendelea kuwabana viongozi wa mamlaka hiyo ni kuwaonea kutokana na fedha wanazokusanya.
“Hawa watu tunaweza tukawa tunawaonea. Ni aibu tuone namna ya kuwasaidia,” amesema.
Kamati hiyo pia, imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalumu kwa hesabu za mamlaka hiyo kutokana na upungufu uliojitokeza katika taarifa za fedha kwa mwaka wa fedha 2015/16.
Awali, wabunge walisema wanapinga taarifa za fedha za mamlaka hiyo kwamba hazijafuata vigezo vya kisheria na mwongozo wa kimataifa.
Mbunge wa Vwawa (CCM), Japhet Asunga amesema hesabu za mamlaka hiyo zina upungufu hali inayotia shaka ilipataje hati safi ya ukaguzi wa hesabu.
Baadhi ya wabunge wamehoji kuhusu utata wa umiliki wa Kampuni ya Maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (Kadco).
Mbunge wa Sikonge (CCM), Joseph Kakunda amewataka wabunge na viongozi wa taasisi hiyo kuwa wazi kwa kuwa kuna vigogo wana masilahi ndani ya Kadco.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Felister Bura amesema kuna jambo katika kampuni hiyo ndiyo maana viongozi wamekuwa wakizunguka kuusema ukweli.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taa, Profesa Ninatubu Lema amesema Kadco imekuwa ikiripoti moja kwa moja serikalini tofauti na viwanja vingine vya ndege nchini.
Wednesday, 30 August 2017
Home
Unlabelled
Wabunge: uwanja wa ndege Dar es salaam unatuaibisha sana, paa linavunja na ni joto sana
Wabunge: uwanja wa ndege Dar es salaam unatuaibisha sana, paa linavunja na ni joto sana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Vat leaching gold processing method is the recently technology that practised in developing nations. In Tanzania vat leaching method w...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment